Title: USHAWISHI NA UTETEZI KATIKA UKUSANYAJI WA RASILIMALI NA RASILIWATU
1USHAWISHI NA UTETEZI KATIKA UKUSANYAJI WA
RASILIMALI NA RASILIWATU
- Imeandaliwa na
- Alex Mayunga
- alexmayunga_at_gmail.com
- Simu 0713 547996
2Tafsiri
- Ushawishi(Lobbying) na Utetezi (Advocacy) ni
dhana zinazotumika pamoja na wanaharakati wengi. - Utetezi ni kupigia debe ama kuunga mkono masuala
ambayo unayaamini - Ushawishi ni mchakato unaobuniwa ili kuepika
mawazo ya wafanya maamuzi ili kupata uungwaji
mkono wa programu ama mkakati . - Maamuzi haya huweza kuwa ya kisera, mkakati,
sheria ama rasilimali. - Ushawishi unalenga kuleta mabadiliko ya kimaslahi
ama matakwa ya wadau mbalimbali ili yaendane na
matakwa ya kikundi husika kama vile Asasi,
Mtandao wa asasi n.k
3UCHAMBUZI WA NGUVU,UDHAIFU, FURSA NA VIKWAZO
KATIKA AZISE/MITANDAO MBALIMBALI.
- NGUVU
- q      Uzoefu wa shughuli za asasi za kiraia
- q      Uwezo mkubwa unaotokana ushiriki mkubwa
wa warsha, semina na makongamano mbalimbali. - q      Timu ndogo lakini zenye watendaji wa
kujitolea. - q      Mazingira ya kijiografia.
- q      Kuwa na mtandao mpana wa taarifa na
shughuli, - q      Kuwa karibu na wadau mbalimbali kama
idara, taasisi za serikali, washirika wa
maendeleo n.k - q      Mtazamo chanya wa wadau juu ya umuhimu wa
uwepo wa AZISE na Mitandao - Â
4UCHAMBUZI WA NGUVU,UDHAIFU, FURSA NA VIKWAZO
KATIKA AZISE/MITANDAO MBALIMBALI.
- UDHAIFU
- q      Ukosefu wa Rasilimali
- Mf. Fedha, vitendea kazi, watendaji
wenye ujuzi na uzoefu - q      Mifumo ya upatikanaji wa Viongozi. Mfano
Kupigiwa kura ama kuteuliwa bila kuzingatia
vigezo. - q      Kutokuwa na viwango vinavyotambulika vya
viongozi wa AZISE - q      Uchanga wa baadhi ya AZISE
- q      Kutamani kutumia kila fursa
inayopatikana.
5UCHAMBUZI WA NGUVU,UDHAIFU, FURSA NA VIKWAZO
KATIKA AZISE/MITANDAO MBALIMBALI.
- FURSA
- Kuwa na mitandao na mashirika mengi yanayofana
kimalengo na dira. - Uwepo wa wadau mbalimbali kama viongozi,
wafanyabiashara na wadau wa maendeleo .
6UCHAMBUZI WA NGUVU,UDHAIFU, FURSA NA VIKWAZO
KATIKA AZISE/MITANDAO MBALIMBALI.
- VIKWAZO
- Kukosa uungwaji mkono wa moja kwa moja na wadau
muhimu. - Mtazamo hasi wa jamii juu ya AZISE.
- Hofu ya utendaji mbovu wa baadhi ya asasi.
- Ushindani mkubwa wa AZISE/MITANDAO inayofanana.
- Ukubwa na uwezo wa kirasilimali na rasiliwatu.
- Hofu ya ukosefu wa uadilifu kwa baadhi ya
watendaji wa baadhi ya wadau wa maendeleo. - Tofauti za shabaha kati ya AZISE na Wadau wa
Maendeleo. -
7KWA NINI STADI ZA USHAWISHI NI MUHIMU?
- Kuwa na stadi muhimu za ushawishi kunatuwezesha
kuweza kuwekeza zadi katika maeneo ambayo tuna
nguvu, kurekebisha udhaifu wa kiasasi, kutumia
vizuri fursa zilizopo na kusaka nyingine na
kikubwa zaidi kuepukana na vikwazo. - Kumbuka si kila changamoto katika AZISE /
Mitandao zinasababishwa na Ufinyu wa Rasilimali
na Rasiliwatu.
8MAMBO MUHIMU KATIKA KUKUSANYA RASILIMALI
- Mingi ya miradi au shughuli ina gharama. Baadhi
itahitaji kiasi kikubwa cha rasilimali na mengine
kiasi kidogo cha rasilimali au mikakati kidogo ya
kukusanya rasilimali. - Mambo ya Kuzingatia
- Makisio ya gharama kwa ajili ya shughuli/mradi.
- Wadau ambao wanaweza kuchangia wataalamu, vifaa
au/na pesa. - Mpango madhubuti wa kukusanya rasilimali/rasiliwa
tu katika maeneo yenye upungufu. - Mchango wa Washiriki ama watu watakaonufaika na
mradi/shughuli
9DONDOO MUHIMU ZA USHAWISHI WA KUKUSANYA
RASILIMALI / RASILIWATU
- Kabla ya kukutana na mdau wa maendeleo kwa ajili
ya kuomba rasilimali ni muhimu kujiuliza mawasli
yafuatayo. - Kwa nini tunamfuata mdau A, B na C na sio D?
- Tunaweza kupata mdau wa kuunga mkono
wazo/mradi/shughuli yetu? - Mdau anajua lolote kuhusiana na asasi/mtandao
wetu na shughuli zake? - Tunajua anajishughulisha na nini, maeneo ya
kipaumbele, shabaha na malengo yake? - Nani ataratibu zoezi la ushawishi inapofikia
hatua ya kuwasilisha maombi yetu? - Mdau anategemea nini toka kwetu?
- Kitu gani hasa tunataka kuomba?
10DONDOO MUHIMU ZA KUKUSANYA RASILIMALI
- 8. Hoja gani tunapaswa kujenga?
- 9. Tunajua shirika ama watu wa karibu wa mdau
ambaye wanaweza kumshawishi? Mf. Mbunge, Diwani,
Meya n.k - 10. Kiasi gani cha rasilimali/rasiliwatu
tunapaswa kuomba? Kiasi maalum ama makisio? - 11. Kuna sababu ya kutokuomba kitu chochote cha
ziada? kama vile mafunzo, vitendea kazi n.k. - 12. Tunataka kuambata na kitu chochote
kinachooneha mafanikio yetu Mfano Ripoti ya
miradi iliyofanikiwa, Barua za pongezi toks kwa
wadau wengine, Majina ya walezi ama wajumbe wa
Bodi ya Udhamini n.k - Â
-
11IPI NI NJIA BORA YA KUKUSANYA RASILIMALIMBINU
YA USHIRIKELI au HOJA?
- USHIRIKELI
- Onesha katika mawasilisho yako na jinsi
unavyowasilisha kwamba unaamini unachokisema na
umejiridhisha kwamba ni muhimu. Kwa njia hii
unaweza kumfanya Mdau wa Maendeleo kuvutika na
kujaribu kuvaa viatu vyako. - Kuwa makini usije ukatumia hisia nyingi
ukaonekana unaomba hisani au kuonewa huruma.
Unaweza kuonekana mwenye kuhitaji sana, usiye
mkweli au usiye na utaalamu. - HOJA
- Mbinu hii inakupasa uwe mjengaji mzuri wa hoja
zenye mashiko kuonesha unajua umuhimu wa mradi
wako. Usijikite kwenye kutoa ahadi ila onesha
jinsi gani unaweza kutekeleza mradi/shughuli yako -
12TUNAWEZAJE KUJENGA MAHUSIANO NA ASASI ZENYE
FALSAFA TOFAUTI?
- Kujenga uhusiano na mashirika ambayo
tonatofautiana nayo katika falsafa ni jambo jema. - Inaongeza sifa kwa asasi, kuongeza uwezekano wa
mafanikio katika baadhi ya maeneo mnayofanana na
kuvutia washirika wa maendeleo wapya. - Hii huweza kufanikiwa iwapo asasi yenu itafanya
ushirika kwa kuvutiwa na masuala ya msingi na
sio haiba za watu. - Usiwashambuie watu unatofautiana nao Hoji
wanayosimamia lakini usiwashambulie. - Jadiliana nao kirafiki na jikite zaidi kwenye
masuala muhuimu. - Kinyume chake tatengeneza maadui ambao pengine
ungeweza kushirikiana nao siku za usoni. - Alika watu toka asasi tofauti katika matukio yenu
-
Ahsanteni!